Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 20:41

Pakistan yatangaza ulinzi zaidi kwa waziri mkuu wa zamani


Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan (Picha: Reuters, Mohsin Raza)
Waziri mkuu wa zamani wa Pakistan, Imran Khan (Picha: Reuters, Mohsin Raza)

Pakistan imetoa amri ya kuongezwa kwa ulinzi kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan, siku moja baada ya kutoa madai kwenye mkutano wa hadhara kwamba kuna mipango ya kumuua.

Ofisi ya waziri mkuu wa sasa wa Pakistan, Shehbaz Sharif, Jumatatu imeeleza kwamba imevielekeza vyombo vya serekali kuu na jimbo kutoa ulinzi mkali kwa kiongozi huyo wakati anapojitokeza katika mihadhara ama shuguli zozote.

Chama cha Khan cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI ) kimepanga mikutano mikubwa ya kuipinga serekali kote nchini toka mapema mwezi uliopita wakati kiongozi huyo alipo ondolewa madarakani baada ya bunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye.

Imran Khan alisikika akisema Jumapili usiku katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika mji wa kati wa Faisalabad kwamba mipango ndani nan je ya Pakistan inafanyika kumuua.

XS
SM
MD
LG