Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:47

Pakistan yasitisha kuwafukuza wahamiaji wa Afghanistan


Pakistan imesitisha kuwafukuza wahamiaji wasio na vibali kutoka Afghanistan baada ya majadiliano na mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi.

Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kuhudumia Wakimbizi, au UNHCR, amemaliza ziara yake ya siku tatu Jumanne na kutoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kupata suluhisho la muda mrefu kwa Waafghanistan nchini Pakistan.

Taarifa ya UNHCR baada ya ziara hiyo imesema, “Grandi alishukuru kuondolewa mpango haramu wa kuwarejesha makwao wageni na kuhakikisha kwamba usitishwaji wake utaendelea.

Afisa mkuu wa Pakistani ambaye alikuwa na ufahamu kuhusu mikutano ya Grandi na viongozi wa Islamabad alithibitisha kwa VOA kwamba Pakistan ilisitisha kuhamisha Waafghanistan.

Forum

XS
SM
MD
LG