Hatua hiyo imechukuliwa baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Taliban Amir Khan Muttaqi, kuahidi wakati wa mkutano wa Alhamisi kati yake na kaimu balozi wa Islamabad mjini Kabul, kwamba utawala wa Taliban hautaruhusu visa vya kigaidi dhidi ya Pakistan kufanyikia kwenye mchanga wa Afghanistan.
Hayo ni kwa mujibu wa afisa wa Pakistan aliyezungumza na VOA kwa masharti ya kutotambulishwa kwa kuwa hajaruhusiwa kuzungumza moja kwa moja na vyombo vya habari. Afisa wa mpakani wa Pakistan amedhibitisha kwamba wafanyakazi wa uhamiaji na usalama wameagizwa warejee kwenye ofisi zao zilizopo kwenye mpaka huo.
Forum