Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 22, 2025 Local time: 13:06
VOA Direct Packages

Paetongtarn Shinawatra atangaza kuwania uwaziri mkuu wa Thailand


Paetongtarn Shinawatra, binti ya aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand,Thaksin aliyetangaza kuwania wadhifa huo kwenye uchaguzi ujao.
Paetongtarn Shinawatra, binti ya aliyekuwa waziri mkuu wa Thailand,Thaksin aliyetangaza kuwania wadhifa huo kwenye uchaguzi ujao.

Paetongtarn Shinawatra Jumatano amethibitisha nia yake ya kuwania uwaziri mkuu wa Thailand akiahidi kuongeza malipo ya kila siku pamoja na kutoa fedha kama zawadi kwa watu wote wa Thailand.

Familia yake yenye sifa kubwa katika siasa nchini humo itajitosa kwenye uchaguzi wa Mei 14, ambao ni muhimu kwa vyama vya demokrasia kuchukua udhibiti tena, kutoka kwa utawala wa kijeshi. Thailand imekumbwa na mapinduzi ya kijeshi katika miaka ya karibuni, mawili yakiwa dhidi tawala za mawaziri wakuu kutoka familia ya Shinawatra.

Ghasia za mitaani pia zimeshuhudiwa wakati serikali zilizochaguliwa kwa njia ya kura zikianguka haraka kufuatia mivutano kati ya wanaharakati wa demokrasia na wale wanaolinda utawala wa kundi la watu wachache mashuhuri wa kikonsavative. Mkuu wa zamani wa jeshi Prayuth Chan-ocha mwenye umri wa miaka 69 ameongoza serikali inayoungwa mkono kijeshi kufutia mapinduzi ya 2014 dhidi ya serikali ya Yingluck Shinawatra.

XS
SM
MD
LG