Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 26, 2024 Local time: 11:21

Marekani yasema kuchoma Kurani si Umarekani


Padre Terry Jones.
Padre Terry Jones.

Serikali ya Marekani inasema mipango ya padri mmoja wa Florida kuchoma moto vitabu vya Kurani kuadhimisha Sep. 11 ni kinyume na maadili ya Marekani.

Serikali ya Marekani inasema mpango wa padri mmoja wa jimbo la Florida kuchoma moto vitabu vya Kurani kama maadhimisho ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11 "inachukiza" na si "Umarekani."

Maafisa wa serikali wanasema padri huyo wa Florida na wafuasi wake wana haki ya kikatiba kuchkua hatua hiyo, kama vile ambavyo wapinzani wa vita vya Marekani wanavyochoma bendera za taifa katika maandamano.

Lakini wanasema wana matumaini kuwa kanisa hilo litafikiria tena kuchukuwa hatua hiyo, na kujaribu kutafuta njia nyingine ya kuadhimisha kumbukumbu ya September 11 bila kuchukuwa hatua ambazo zinaweza kuchochea upinzani dhidi ya Marekani na kusababisha ghasia nje ya nchi.

Katika ujumbe uliokuwa na maneno makali tangu mipango ya padri wa kanisa la kiinjili huko Florida, Terry Jones, kutangazwa, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, P.J. Crowley alisema hatua hiyo inachukiza, haikubaliki, na haifai kufanyika.

“Tunadhani vitendo hivi ni vya uchokozi, havina heshima, havistahmiliki, vita leta mgawanyiko na tunafahamu kuwa watu kadhaa wamejitokeza na kupinga kile ambacho padri huyu na wafuasi wake wanataka kufanya. Tungependa kuona Wamarekani zaidi wanasimama kidete na kusema jambo hili halipo katika thamini za kimarekani, kwa kweli ni hatua ambazo ni kinyume na maadili ya kimarekani,” alisema Bw. Crowley.

Bw. Crowley anasema ikiwa mpango wa kuchoma Kurani utafanyika, basi anatumai kuwa watu duniani kote watatambua kuwa kitendo hicho hakiashirii maoni ya wamarekani wengi na wala utamaduni wa Marekani wa ustahmilivu wa kidini.

XS
SM
MD
LG