Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 04, 2024 Local time: 00:51

Alassane Ouattara aapishwa rasmi kuwa Rais wa Ivory Coast


Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, akiwa na ujumbe wa tume ya ulaya kwenye hoteli ya Golf huko Abidjan, May 6, 2011
Rais wa Ivory Coast, Alassane Ouattara, akiwa na ujumbe wa tume ya ulaya kwenye hoteli ya Golf huko Abidjan, May 6, 2011

Baraza la katiba nchini Ivory Coast linasema Alassane Ouattara ataapishwa kama Rais wa n chi hiyo leo Ijumaa.

Mahakama ya juu nchini Ivory Coast jana ilimtangaza bwana Ouattara mshindi wa uchaguzi wa Rais uliofanyika mwaka jana, kwa asilimia 54 ya kura, na kubadilisha uamuzi wake wa awali uliompendelea Rais wa zamani Laurent Gbagbo.

Bwana Gbagbo alitumia maamuzi ya awali kujitangaza mshindi na kung’ang’ania madaraka. Kukataa kwake kuondoka madarakani kulizusha ghasia, mapambano ya madaraka kwa miezi minne na kusababisha vifo vya mamia ya watu na kuwakosesha makazi watu milioni moja.

Bwana Ouattara alichukua madaraka mwezi uliopita, baada ya wafuasi wake kumkamata mpinzani wake bwana Gbagbo katika nyumba yake ya Abidjan kwa msaada wa majeshi ya Umoja wa Mataifa na Ufaransa.

Katika maendeleo mengine hapo jana Alhamis, Marekani ilisema inatoa dola milioni 8.5 nyingine kuwasaidia watu wa Ivory Coast ambao walikimbia nyumba zao wakati wa matatizo. Maafisa wa Marekani wanasema fedha hizo zitatumika kusaidia huduma za afya, maji safi na mahitaji mengine muhimu ya nyumbani.

Marekani inasema ahadi hiyo inafikisha jumla ya dola milioni 43 za msaada ilizozitoa kwa wakimbizi wa Ivory Coast na watu waliokoseshwa makazi ndani ya nchi.

XS
SM
MD
LG