Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:37

Oscar Pistorius apanda kizimbani


Oscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini London
Oscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini London
Mwanariadha wa Afrika Kusini katika michuano ya Olympic Oscar Pistorius alikuwa kwenye mahakama moja ya Pretoria Jumanne ambapo anakabiliwa na mashtaka ya mauaji kwa kumfyatulia risasi na kumwua rafiki yake wa kike, mrembo Reeva Steenkamp. Pistorius atakabiliwa na mapambano makali ya kupata dhamana baada ya jaji kusema kuwa aliyapanga mauaji hayo.

Mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel hakusema chochote wakati wa kusikilizwa kesi hiyo , akitangaza kuwa Oscar Pistorius anashtakiwa kwa mauaji. Tangazo hilo limepelekea mwanariadha huyo wa michuano ya Olympic kulia.

Nel kisha alielezea mtazamo wa mauaji yaliyotokea Februari 14 kwenye nyumba ya Pistorius huko Pretoria.

Picha aliyochora ilikuwa kielelezo: Mlemavu huyo wa miguu yote miwili alishutumiwa kuambatanisha viungo vyake bandia, alitembea mita saba kuelekea karibu na bafu na kumfyatulia risasi mara nne Reeva Steenkamp kupitia mlango ambao ulikuwa umefungwa. Nel aliiambia mahakama kwamba Pistorius kisha alivunja mlango kutoka nje na kuubeba mwili wa mpenzi wake hadi chumba cha chini na alimuita rafiki mmoja akimweleza kuwa alidhani Steenkamp alikuwa mwizi.

Dai hilo Nel alisema linaonyesha kwamba Pistorius alipanga mauaji.
Mwendesha mashtaka Desmond Nair alikubali akisema hakuna shaka yalikuwa mauaji ya kukusudia.

Wakili wa utetezi Barry Roux aliangalia mtazamo tofauti akielezea kuwa hayo si mauaji.
XS
SM
MD
LG