Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Julai 14, 2024 Local time: 22:21

Operesheni ya kuondoa mafuta kutoka meli chakavu huko Yemen imeanza;Inasema UN


Meli ya FSO Safer ikionekana kwenye pwani ya bahari ya Sham huko Yemen. June 12, 2023.
Meli ya FSO Safer ikionekana kwenye pwani ya bahari ya Sham huko Yemen. June 12, 2023.

Meli ya FSO Safer ilikuwa ikizungumziwa kwa miaka kadhaa  kutokana na maombi kutoka Umoja wa Mataifa na mashirika ya mazingira ambao walionya kuwa ukosefu wa matengenezo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen inamaanisha kuwa meli hiyo ilikuwa katika hatari ya kumwaga mafuta

Umoja wa Mataifa umesema Jumanne kwamba operesheni iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya kuondoa mafuta kutoka kwenye meli chakavu ya mafuta katika pwani ya bahari ya Sham huko Yemen imeanza.

Meli ya FSO Safer ilikuwa ikizungumziwa kwa miaka kadhaa kutokana na maombi kutoka Umoja wa Mataifa na mashirika ya mazingira ambao walionya kuwa ukosefu wa matengenezo wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Yemen inamaanisha kuwa meli hiyo ilikuwa katika hatari ya kumwaga mafuta mara nne zaidi ya janga la 1989 Exxon Valdez huko Alaska.

Taarifa ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa imesema mafuta hayo yatahamishiwa katika meli mpya ya mafuta ya Yemen katika mchakato ambao ulitarajiwa kuchukua siku 19.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema kazi hiyo ni hatua muhimu katika kuepusha janga la mazingira kwa kiwango kikubwa.

Forum

XS
SM
MD
LG