Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 03, 2024 Local time: 05:42

OPEC+ yakaribisha Namibia kujiunga kama mwanachama mpya


Nembo ya OPEC nje ya ukumbi wa mkutano wa Algiers, Algeria. Septemba 28, 2016
Nembo ya OPEC nje ya ukumbi wa mkutano wa Algiers, Algeria. Septemba 28, 2016

Kundi la mataifa yanayozalisha mafuta la OPEC+, baada ya kupoteza uanachama wa Angola miongoni mwa wengine katika miaka ya karibuni sasa linalenga kuikaribisha Namibia kujiunga nalo

Hilo limefanyika wakati taifa hilo likijianda kuwa mzalishaji wa nne kwa ukubwa barani Afrika ndani ya muongo mmoja ujao, mtaalam wa kiviwanda ameambia Reuters. Makampuni ya mafuta ya TotalEnergies na Shell katika miaka ya karibuni yamegundua mafuta yanayokisiwa kuwa mapipa bilioni 2.6 nchini humo.

Angola inapanga kuanza uzalishaji wa mafuta ya kibiashara ifikapo 2030. Taarifa zimeongeza kuwa lengo kubwa la OPEC+ kwa sasa ni kukaribisha Namibia kwenye mkataba wa ushirikiano, ambao utafungua milango ya mazungumzo ya muda mrefu kuhusu soko la mafuta. Brazil ilijiunga kwenye mkataba huo Januari mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG