Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:07

Olaf Scholz aidhinishwa rasmi kama Kansela wa Ujerumani


Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela mpya wa Ujerumani Olaf Scholz

Bunge la Ujerumani limemchaguwa Olaf Scholz kama kansela wa tisa wa baada ya vita vya pili vya dunia na hivo anafunguwa ukurasa mpya wa utawala baada ya uongozi wa miaka 16 wa Angela Merkel.

Serikali ya Scholz inachukuwa hatamu za uongozi kwa matumaini makubwa ya kuifanya Ujerumani kuwa ya kijani na ya haki zaidi ikiongoza katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa. Hata hivyo serikali mpya inakabiliwa na changamoto ya hivi sasa ya kushughulikia kipindi kigumu zaidi cha janga la virusi vya corona nchini.

Jumatano, Scholz amepata uungwaji mkono wa wabunge 395. Muungano wake wa vyama vitatu una viti 416 katika bunge lenye viti 736.

Scholz mwenye umri wa miaka 63 anaeiga mwenendo wa aliyemtangulia Merkel ameleta pamoja serikali ya mseto ya vyama vitatu na ya kwanza ya usawa wa jinsia. Rais Frank Walter Steinmeier amemteua rasmi Scholz kuwa kansela wa Ujerumani.

XS
SM
MD
LG