Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:26

Odinga na Musyoka waungana 2013


Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
Mahasimu wakuu wa kisiasa nchini Kenya, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu Rais, Kalonzo Musyoka, Jumanne jioni walitia saini makubaliano ya kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu ujao na hatimaye kuunda serikali ya muungano.

Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya kutia saini makubaliano ya kushirikiana kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwakani.

please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:10 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Katika sherehe zilizohudhuriwa na watu mbali mbali kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi, bwana Odinga na bwana Musyoka, pia walimshirikisha kiongozi wa chama cha FORD Kenya, Moses Wetangula ambaye pia ni waziri wa biashara. Vile vile kuna vyama vya kisiasa vingine 11 vilivyoshirikishwa katika makubaliano hayo lakini baadhi yake ni vyama vya watu binafsi.

Akizungumza katika sherehe hizo Musyoka alisema hisia zake za kisiasa sasa zimebadilika kumhusu Raila Odinga “ kama ningekuwa mtu wa kushikilia ghadhabu hasira nisingekuwa hapa leo na mheshimiwa Odinga lakini tunasema hayo sasa iko nyuma yetu ni lazima tuyagange yaliyo mbele ili vile dada yetu Ngilu amesema juu ya shida ya wananchi kutokuwa na kazi kutokuwa na ajira wananchi kulala hoi na wengine wanalala hai”.

Wakati huo huo Waziri Mkuu Odinga alishutumu vikali miungano ya kisiasa inayojengwa kwenye misingi ya kikabila. Alisema “ vyama vishindane kwa sera sio kwa msingi ya ukabila ati kabila hii iungane na kabila hii inyakue utawala, nataka kuona kama mwanasiasa wako kwenye mstari wa mbele kuunganisha wakenya”.

Ikiwa imesalia takribani miezi miwili kabla ya uchaguzi kufanyika kumekuwa kumekuwa na harakati za wanasiasa kukamilisha miungano ya kisiasa kabla ya muda wa mwisho wa kuwasilisha mikataba hiyo katika ofisi ya vyama vya msajili wa kisiasa.
XS
SM
MD
LG