Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 15, 2025 Local time: 15:07

Odinga ataka maafisa 12 wa IEBC wafungwe jela


Raila Odinga
Raila Odinga

Kiongozi wa Muungano wa Nasa nchini Kenya Raila Odinga anataka maafisa 12 wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IOEBC) wafungwe jela.

Maafisa hao ambao wametajwa na muungano wa upinzani kuwa wanahusika na kuvuruga uchaguzi wa urais wa Agosti 8 uliobatilishwa, Odinga anataka wafungwe baada ya kufukuzwa kazi.

Odinga amesema maafisa hao 12, akiwemo kamishna Abdi Guliye na Boya Molu pamoja na mtendaji mkuu wa IEBC Ezra Chiloba, manaibu wake wawili Betty Nyabuto na Marjan Hussen Marjani, lazima waadhibiwe kwa kile Nasa ilichokieleza kama “kudhuru uhuru wa matakwa ya watu.”

“Wote hao walioendesha uchaguzi wa mwisho lazima waangalie uchaguzi unaofuata wakiwa jela , siyo kutoka ofisi za IEBC,” Odinga amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwenye jengo la Okoa Kenya Secretariat huko Lavington Jumatatu mchana.

Aliendelea kusema: “ Hatutaki tu uchaguzi kama jina la uchaguzi. Tunataka uchaguzi uendeshwe na wanaume na wanawake wenye uadilifu, siyo kina Chilobas, Guliyes, Kassaits wa ulimwengu huu.”

Maafisa wengine waliotajwa na Odinga ni wakurugenzi Immaculate Kasait (Uchaguzi), Praxedes Tororey (Sheria), James Muhati (ICT) na Moses Kipkosgey, mshauri wa sheria wa Chiloba.

XS
SM
MD
LG