Ikiwa chini ya wiki tatu kabla ya uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya, Waziri Mkuu aliyepo madarakani Raila Odinga anaongeza juhudi na matumaini yake ya kushinda katika mzunguko wa kwanza. Huku siku za uchaguzi zikikaribia Odinga anaongeza ukosoaji wake dhidi ya mpinzani wake mkuu kwa matumaini ya kuepuka upigaji kura wa mzunguko wa pili.
Odinga na Naibu Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta ni wagombea urais wanaoongoza. Lakini katika kundi la wagombea wanane waliopo utafiti unaonyesha hakuna mgombea yeyote atayepata nusu ya kura katika mzunguko wa kwanza. Jambo hilo litasababisha kuwepo na mzunguko wa pili kati ya wagombea wawili wa juu.
Licha ya maoni ya utafiti wapanga mikakati wa Odinga wana imani kuwa anaweza kushinda katika mzunguko wa kwanza.
Ni operesheni kubwa. Kampeni ya Odinga inajumuisha timu nane zinazotangulia katika mikutano ya hadhara na maelfu ya watu wa kujitolea. Wiki iliyopita walipanga mikutano iliyojaa watu kwenye eneo lote la jimbo la Pwani.
Wanachama wa Bwana Odinga wa Coalition for Reforms and Democracy waliongeza mashambulizi yao dhidi ya bwana Kenyatta wakiwakumbusha wapiga kura kwamba mpinzani huyo bado yupo chini ya shutuma za mahakama ya kimataifa ya uhalifu-ICC.
Bwana Kenyatta na mgombea wake mwenza William Ruto wote wanashtakiwa katika kuhusika na ghasia ambazo zilitokea kote Kenya baada ya uchaguzi wa urais uliokuwa na utata mwaka 2007. Bwana Kenyatta amerudia kukanusha mashtaka ya ICC na alisema kwenye mdahalo wa urais wa jumatatu kuwa kesi hiyo haitaingilia uwezo wake wa kuongoza nchi.
Lakini katika mkutano huko Malindi mgombea mwenza wa Bwana Odinga, Kalonzo Musyoka aliwaonya wapiga kura kwamba kumchagua Bwana Kenyatta kutaharibu sifa ya Kenya kimataifa.