Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 14, 2024 Local time: 23:36

Rais Obama ahutubia Mataifa ya South Pacific


Rais Barack Obama akihutubia kikao cha Mataifa ya South Pacific Vientiane Laos Septemba 6, 2016.
Rais Barack Obama akihutubia kikao cha Mataifa ya South Pacific Vientiane Laos Septemba 6, 2016.

Rais Barack Obama wa Marekani Jumanne alihakikishia mataifa yalioko kwenye eneo la Asia Pacific usaidizi wa Marekani.

Rais Barack Obama wa Marekani Jumanne alihakikishia Mataifa yalioko kwenye eneo la Asia Pacific kuwa usaidizi wa Marekani katika eneo hilo utaendelea kwa muda mrefu kwa kuwa limeonesha maswala mengi yenye umuhimu wa kitiafa.

Wakati akitoa hotuba kwenye mji wa Vientiane nchini Laos, Obama alisema Marekani inatambua kwamba eneo la Asia Pacific lina umuhimu mkubwa katika karne ijayo kwa Marekani na ulimwengu kwa ujumla.

Obama alikuwa akihutubia takriban watu 1,000 kwenye ukumbi wa kitaifa wa kitamaduni wa Lao siku moja baada ya kuweka historia kama rais wa kwanza wa Marekani kufanya ziara nchini humo akiwa ofisini.

XS
SM
MD
LG