Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 06:38

Obama, Romney wakamilisha kampeni zao


Rais Barack Obama akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake mjini Madison Wisconsin
Rais Barack Obama akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake mjini Madison Wisconsin
Wagombea wawili wakuu katika mashaindano hayo rais Barack Obama na mrepublican Mitt Romney wanasafiri katika majimbo kadhaa yenye ushindani mkubwa katika kampeni zao za kufa na kupona kuwaraia wapiga kura kujitokeza kwa wingi, kwa vile uchunguzi wa maoni unaonesha wako sare katika kinyan’ganyiro hicho.

Kufuatana na wachambuzi wa mambo mshindi atamuliwa kutokana na idadi ya watu watakao jitokeza hapo Jumanne na nani atakae ibuka mshindi katika majimbo saba yenye ushindani mkubwa, kwani katika uchaguzi wa Marekani rais huchaguliwa na wajumbe wa majimbo 50.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:29 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Moja wapo ya jimbo muhimu ni Florida ambako inasemekana rais Obama anaongoza akiongoza kwa idadi ndogo sana na alilitembelea jimbo hilo Jumapili akisema,

“Kwa nyingi ambao hamjaamua au marafiki zenu au majirani zenu wanaojaribu kufikiria wampigiye kura nani, hii si suala la chaguo kati ya wagombea wawili au vyama viwili bali, ni chagua kati ya itikadi mbili tofauti juu ya mustakbal wa Marekani. Ni chagua kati ya kurudi nyuma na sera zilizoporomosha uchumi wetu au kuimarisha jamii ya tabaka la kati kwa misingi ya sera zilizotokomboa kutoka mzozo wa awali.”

Mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney alitembelea jimbo la mashariki la Pennsylvania ambako uchunguzi wa maoni unaonesha rais anaongoza.
Hata hivyo Romney alisema bado kuna wakati wa kupiga kura kufuta njia mpya.

“Tuna siku mbili tu kabla ya kufungua ukurasa mpya. Siku mbili kabla ya mwanzo mpya. Imani yangu ni kwamba tutakuwa na siku bora zaidi huko mbele, lakini si kwa misingi ya ahadi tupu bali mipango kabambe na matokeo yaliyothibitishwa.”

Siku ya Jumatatu rais Obama anatembelea Wisconsin na Iowa na kukamilisha kampeni kwa mkutano Ohio kabla ya kurudi nyumbani Chicago ambako atasubiri matokeo ya Jumanne usiku.

Kwa upande wake Mitt Romney anatembelea Florida, Virginia, Ohio na New Hampshire kabla ya kurudi nyumbani Boston kusubiri matokeo.

Kampeni ya Romney
Kampeni ya Romney
Mbali na uchaguzi huo wa rais, kuna viti 435 vya Baraza la Wawakilishi la Bunge la Marekani vinagombaniwa pamoja na theluthi moja ya viti vya Baraza la Senet yani viti 33. Baraza la Senet linashikiliwa na wademokrats kwa wakati huu, huku Baraza la Wawaklilishi linashikiliwa na warepublican.

Zaidi ya hayo kuna majimbo 11 yenye uchaguzi wa magavana mbali ya uchaguzi wa mabunge ya majimbo 50 na serikali za mitaa.

please wait

No media source currently available

0:00 0:09:11 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kadhalika, wapiga kura wanatazamiwa kupiga kura ya maoni juu ya masuala mbali mbali kuhusiana na majimbo au wilaya yao. Masuala hayo ni yale yanafikishwa kwa wananchi baada ya mabunge ya majimbo au mabaraza ya miji kuidhinisha au kushindwa kukubaliana na kuna upande usoridhika.

Moja wapo ya suala linalofuatwa kwa makini kote nchini ni kura ya maoni ya jimbo la Maryland kuidhinisha ndoa ya watu wa jinsia moja katika jimbo hilo. Pendekezo kama hilo lilishindwa tayari katika majimbo manne katika uchuaguzi ulopita.

Marekani wapiga kura wanaruhusiwa katika majimbo mengi kupiga kura kabla ya siku ya kura ikiwa wanaudhuru au hawatakuwepo katika wilaya zao za kupiga kura, hata hivyo katika uchaguzi huu katika lengo la kupunguza milongo ya wapiga kura siku ya uchaguzi watu wamekubaliwa kupiga kura mapema.

Na hata kabla ya uchaguzi kuanza rasmi mashtaka yamefikishwa mbele ya mahakama huko Florida na Ohio juu ya kasoro za utaratibu wa uchaguzi.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:16 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Wananchi wa Marekani watapumua siku ya Jumanne baada ya kupiga kura kutokana na mikutano ya kampeni za uchaguzi isiyomalizika iliyofanyika kwa mwaka mzima, lakini hasa kutokana na matangazo ya kisiasa ambayo pande zote mbili zimekuwa zikitangaza na inakadiriwa kwamba kila mgombea rais ametumia dola milioni 800 katika kampeni zao ikiwa ni rikodi katika historia ya uchaguzi wa Marekani.

Na inakadiriwa dola bilioni moja zilitumiwa na makundi mabli mbali ya kiraia kusaidia wagombea wao.
XS
SM
MD
LG