Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:54

Obama amteua Patraeus kamanda mkuu wa Marekani, Afghanistan


Jenerali David Petraeus, kamanda mkuu wa Marekani, Afghanistan.
Jenerali David Petraeus, kamanda mkuu wa Marekani, Afghanistan.

Rais wa Marekani Barack Obama, amemteua Jenerali David Petraeus, mkuu wa majeshi ya Marekani Iran na Afghanistan kuchukua nafasi ya Jenerali Stanley McChrystal na kuwa kamanda mkuu wa Marekani nchini Afghanistan.

Rais wa Marekani Barack Obama, amemteua Jenerali David Patraeus, mkuu wa majeshi ya Marekani Iran na Afghanistan kuchukua nafasi ya Jenerali Stanley McChrystal na kuwa kamanda mkuu wa Marekani nchini Afghanistan.

Rais Obama alisema ingawa ni vigumu sana kupoteza uongozi wa McChrystal, ni uamuzi mzuri kujiuzulu kwake kwa ajili ya usalama wa kitaifa. Alisema matamshi ya McChrystal kwenye makala ya jarida la Rolling Stone hayakufikia kiwango cha nidhamu kinachohitajika kutoka kwa Jenerali anayeongoza.

Jenerali McChrystal alikutana na Rais Obama White House siku ya Jumatano baada ya kuitwa Washington kueleza matamshi yake ya kukejeli uongozi wa utawala wa Obama katika maswala ya Afghanistan.

Kabla hajaondoka Washington, McChrystal alisema maelezo ya makala yaliyochapishwa na Rolling Stone yalikua ni kosa na haikustahili kutendeka.

Katika makala hayo yaliyopewa jina la “The Runaway General”, washauri wa McChrystal wananukuliwa wakimtaja afisa wa cheo cha juu wa Obama kuwa ni “mpumbavu” na mwengine ni “mnyama aliyejeruhiwa”. Makala hayo yalieleza pia kuwa Jenerali huyo alivunjika moyo na mkutano wake wa kwanza na Rais.

XS
SM
MD
LG