Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 12:43

Obama kuhutubia Hanoi huko Vietnam


Rais wa Marekani Barack Obama (L) na Rais wa Vietnam Tran Dai Quang mjini Hanoi, Vietnam.
Rais wa Marekani Barack Obama (L) na Rais wa Vietnam Tran Dai Quang mjini Hanoi, Vietnam.

Rais wa Marekani Barack Obama atahutubia mjini Hanoi siku ya Jumanne akitarajiwa kulenga juu ya kuboresha mahusiano kati ya Marekani na Vietnam na umuhimu wa kujenga majadiliano yenye tija kati ya nchi hizo mbili.

Maafisa wa White House walisema rais atasisitiza umuhimu wa mataifa hayo mawili kujihusisha katika mazungumzo yenye maana pale wanapotofautiana ikiwemo haki za binadamu. Bwana Obama pia atakutana Jumanne na wanaharakati wa makundi ya kiraia pamoja na wajasiriamali vijana.

Siku ya Jumatatu alitangaza kwamba Marekani inaondoa marufuku yake ya silaha ya muda mrefu kwa Vietnam. Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari akiwa na Rais wa Vietnam, Tran Dai Quang, Obama alisema Marekani imeondoa marufuku yote ya uuzaji wa vifaa vya kijeshi kwa Vietnam, ambayo imekuwepo kwa karibu miaka 50, akiongeza kwamba uuzaji bado utahitajika kufikia vigezo vinavyohitajika ikiwemo vyote vya haki za binadamu lakini mabadiliko haya yanaihakikishia Vietnam ina fursa ya kupata vifaa inavyohitaji kwa ajili ya kujilinda yenyewe.

Rais Quang aliikaribisha hatua hiyo kama mwisho wa ukurasa wa maumivu

XS
SM
MD
LG