Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 04:02

Obama kugombea urais 2012


Rais Obama

Tangazo hilo lilitolewa Jumatatu katika tovuti ya YouTube, pamoja na ujumbe wa barua pepe kwa wafuasi wa Bw. Obama ambao amewahakikishia kuwa anajaza karatasi zinazotakiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Rais Barack Obama ametangaza rasmi nia yake ya kuwania awamu ya pili ya urais. Mwandishi wa VOA Dan Robinson anaripoti kwamba tangazo hilo limetolewa wakati Rais Obama anakabiliana na maswala mbalimbali ndani na nje ya nchi, ikiwemo mkakati wa kufufua uchumi wa Marekani.

Tangazo hilo litolewa kwa ukanda wa video Jumatatu katika tovuti ya YouTube, pamoja na ujumbe wa barua pepe kwa wafuasi wake ambao Bw. Obama amewahakikishia kuwa anajaza karatasi zinazotakiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kuanza kukusanya michango kwa ajili ya kampeni yake ya mwaka 2012.

Video hiyo imevuta hisia za wengi kwamba hakuna mahala inapomuonyesha Bw. Obama akitoa taarifa rasmi kuhusu mpango wake wa kugombea muhula mwingine ama kuhusu sera zake.

Badala yake, inaonyesha maoni ya wamarekani waliomuunga mkono rais mwaka 2008, wakieleza kwa nini wanaamini kwamba ni muhimu kwa rais Obama kuchaguliwa tena mwakani.

Kama ilivyokuwa katika uchaguzi wa mwaka 2008, kampeni za kuchaguliwa tena kwa Bw Obama hazitapokea fungu la fedha kutoka serikali kuu. Hili litampa uhuru wa kuchangisha kiasi kikubwa cha fedha kuzidi dola milioni 780 alizopokea mwaka 2008, na wachambuzi wengi wa siasa wanatabiri kwamba atahitaji takriban dola bilioni moja kwa uchaguzi ujao wa mwaka 2012.

XS
SM
MD
LG