Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:20

Obama aendelea kutangaza mpango wake wa kubuni ajira


Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Richmond, huko Virginia kuhusu mpango wake wa kubuni ajira kwa taifa. Septemba 9,2011
Rais wa Marekani Barack Obama akiwahutubia wanafunzi wa chuo kikuu cha Richmond, huko Virginia kuhusu mpango wake wa kubuni ajira kwa taifa. Septemba 9,2011

Rais Obama wa Marekani amewataka wanafunzi wa chuo kikuu huko Virginia kulishinikiza bunge kukubali mpango wake wa kubuni ajira kwa taifa

Rais wa Marekani Barack Obama aliuambia umati wa wanafunzi wa chuo kikuu huko Virginia Ijumaa kulishinikiza bunge kulikubali pendekezo lake la kubuni nafasi za ajira.

Bwana Obama alirudia tena msemo wake wa “pitisha mswada huu” alipoonekana Ijumaa huko Richmond. Akihamasisha mpango wa takribani dola bilioni 450 alioutangaza Alhamis kwenye kikao cha pamoja na bunge. Alisema katika siku zijazo atatangaza mpango wa kupunguza nakisi ambao utafidia gharama za pendekezo lake.

Mpango wa bwana Obama utatoa punguzo la kodi kwa wafanyakazi na wafanya biashara na kufadhili miradi ambayo itawaajiri wafanyakazi wa ujenzi na kutoa nafasi nyingine za ajira. Pendekezo hilo linajumuisha juhudi za kuwarudisha watu kazini na kukarabati barabara, njia za reli, viwanja vya ndege, njia za majini na shule zisizopungua 35,000.

Spika wa bunge John Boehner, kiongozi wa chama cha Repuplican ambaya mara kwa mara anapingana na Rais, alisema pendekezo la bwana Obama inafaa liangaliwe kwa kina.

Mbunge mmoja mwanamke wa chama cha Repuplican na mgombea urais kwa mwaka 2012, Michele Bachmann alisema baada ya hotuba kwamba hakuona hotuba hiyo ilikuwa na mapendekezo yoyote mapya.

Takwimu za karibuni kuhusu ajira zilionesha kubakia katika kiwango kile kile, huku wasi wasi ukiongezeka juu ya uwezekano wa kipindi cha pili cha kudorora kwa uchumi.

Kiwango cha watu wasio na ajira Marekani kipo asilimia 9.1 na takwimu za serikali kuu zinaonyesha kwamba hakuna ajira mpya zilizobuniwa mwezi Agosti. Kiasi cha wafanyakazi milioni 14 hawana ajira na mamilioni zaidi wanafanya kazi za muda au kazi ambazo haziendani na kiwango chao cha elimu.

XS
SM
MD
LG