Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 23:50

Obama: Russia lazima ishirikiane na kiongozi mpya Ukraine


Viongozi wa G7 katika mkutano wao Brussels, Juni 5
Viongozi wa G7 katika mkutano wao Brussels, Juni 5
Rais Barack Obama wa Marekani amesema Rais Vladimir Putin wa Russia ni lazima atambue na kushirikiana na uongozi mpya wa serikali ya Ukraine uliochaguliwa, na kuwacha "uchokozi" katika eneo la mpaka wao, ama sivyo atakabiliwa na vikwazo kutoka kwa nchi wanachama wa kundi la G 7.

Pande zote zinakubali kuwa Russia ni lazima ibadili mwenendo wake, na ziliungana kutishia vikwazo vipya ambavyo vitalenga maeneo yote ya uchumi wa Russia.

"Tutakuwa na nafasi ya kuona Bw Putin anafanya nini katika kipindi cha wiki mbili, tatu, nne zijazo, na kama ataendelea kuwa katika mkondo anaochukua hivi sasa, basi tumeshaonyesha ni hatua za namna gani tuko tayari kuchukua," Obama alisema katika mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron mwishoni mwa mkutano wa G7 huko Brussels, Ubelgiji.

"Russia inahitaji kuchukua fursa hii," alisema Obama. "Russia inahitaji kutambua kuwa Rais-mteule (Petro) Poroshenko ni kiongozi halali wa Ukraine na ashirikiane na serikali ya Kyiv."

Obama alitoka katika mkutano huo wa siku mbili wa G7, akisema ilikuwa ni fursa kwa viongozi waliokutana kuhakikisha wako pamoja katika mkakati wa kusonga mbele katika maswala ya Ukraine.
XS
SM
MD
LG