Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:13

Obama awataka wamarekani kulishinikiza bunge juu ya sheria ya bunduki


Watu wamekusanyika jirani na eneo lililotokea ufyatuaji risasi huko Roseburg, Oregon
Watu wamekusanyika jirani na eneo lililotokea ufyatuaji risasi huko Roseburg, Oregon

Rais Barack Obama akiwa amekasirika aliwataka wamarekani walishinikize bunge kupitisha sheria ya bunduki kwa kutumia mifano hai, baada ya mtu mmoja mwenye silaha kuwauwa watu 10 na kuwajeruhi saba kwenye chuo kimoja cha Oregon siku ya Alhamis.

Bwana Obama alionekana kwenye televisheni mwenye majonzi saa kadhaa baada ya ufyatuaji huo kutokea akilikumbusha taifa kwamba wamarekani wengi ikiwemo wamiliki wa bunduki wanaoheshimu sheria, wanataka sheria kali kuwekwa. Alisema wamarekani wamekuwa kama wamekufa ganzi kwa kile ambacho kimekuwa jambo la kawaida nchini Marekani, ufyatuaji risasi holela uliofuatiwa na taarifa yake ya White House na kujibiwa na wale ambao wanapinga udhibiti zaidi wa bunduki.

Alisema hoja kwamba bunduki nyingi zinawaweka watu salama haiwezi kufanyika kwa kutazamana.

Rais Barack Obama akizungumzia tukio la Oregon
Rais Barack Obama akizungumzia tukio la Oregon

Bwana Obama aliwaomba wapiga kura kukumbuka nani anaunga mkono na nani anapinga sheria ya bunduki katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Taarifa zaidi za ufyatuaji risasi holela kwenye chuo cha Umpgua mjini Roseburg katika jimbo la Orego nchini Marekani bado haziko wazi.

Lakini mkuu wa polisi katika halmashauri ya Douglas, John Hanlin alithibitisha kwamba mfyatuaji risasi aliuwawa wakati akipambana kwa risasi na polisi. Bwana Hamlin alisema mfyatuaji risasi mwenye umri wa miaka 20 alifyatua risasi katika moja ya madarasa na polisi haraka walijibu kufuatia simu ya dharura.

Mkuu huyo wa polisi alisema idara nyingi za vyombo vya usalama ikiwemo FBI wanashiriki katika uchunguzi. Maafisa wanahakikisha eneo la chuo liko salama na wanaangalia kile kilichochochea tukio hilo.

Maafisa wa polisi wa Oregon
Maafisa wa polisi wa Oregon

Maafisa wanaamini mtu huyo aliyekuwa na silaha alikuwa akilifahamu vyema eneo na majengo ya shule. Pia walisema aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuhusu kile alichokuwa akipanga kufanya. Mtu mmoja aliyenusurika aliwaambia waandishi wa habari kwamba mfyatuaji risasi alidai kujua dini ya kila mmoja darasani kabla ya kuanza kufyarua risasi.

Lakini maafisa wanaamini hii ilikuwa kesi ya ugaidi wa ndani usiokuwa na ushirikiano wowote na kundi la kimataifa.

Bwana Hanlin aliliita tukio la Alhamis “mshtuko mkubwa” kwa halmashauri hiyo tulivu iliyo kijijini mahala ambako wakazi wachache hawajulikani.

XS
SM
MD
LG