Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 12:06

Obama awataka vijana wa YALI kuongoza mabadiliko


Rais Barack Obama akizungumza na vijana wa YALI mjini Washington, Aug. 3, 2015
Rais Barack Obama akizungumza na vijana wa YALI mjini Washington, Aug. 3, 2015

Rais Barack Obama aliwataka vijana wa Afrika kushiriki zaidi katika ujasiriamali na shughuli za maendeleo katika mataifa yao kama sehemu ya ajenda kuu ya kuendeleza bara la Afrika.

Bwana Obama alisema hayo Jumatatu mjini Washington wakati alipozungumza na vijana wa Afrika wanaoshiriki katika mpango wa vijana viongozi wa Afrika-YALI ambao unawakutanisha vijana wa Afrika mjini Washington.

Katika hotuba iliyogusia mambo mengi pamoja na kipindi kirefu cha maswali na majibu Rais Obama alisema vijana ni lazima waongoze mabadiliko katika jamii na lazima wawe jasiri kwa sababu katika jamii nyingi kuna desturi ambazo hazikubali baadhi ya mabadiliko hasa yanayohusu thamini za jamii.

Washiriki katika mkutano wa YALI, Washington DC
Washiriki katika mkutano wa YALI, Washington DC

Pia Rais Obama alitangaza hatua kadhaa za kupanua mpango wa YALI ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kwa kituo cha kanda cha YALI huko nchini Ghana mwaka ujao ambapo vijana wa kimarekani wapatao 80 watashiriki katika mpango kama huo kwenda barani Afrika na kwamba mwaka ujao mpango wa YALI utapanuka zaidi na kushirikisha vijana 1,000 kutoka Afrika. Mwaka huu mpango wa YALI umewashirikisha vijana 500 kutoka nyanja mbali mbali barani Afrika

XS
SM
MD
LG