Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:12

Obama atoa hotuba kuhusu hali ya kitaifa


Rais Obama akiwapungia mkono wabunge na watu mbali mbali ndani ya bunge kabla ya kutoa hotuba yake ya hali ya kitaifa
Rais Obama akiwapungia mkono wabunge na watu mbali mbali ndani ya bunge kabla ya kutoa hotuba yake ya hali ya kitaifa

Rais wa Marekani Barack Obama alitoa hotuba yake ya hali ya kitaifa jana huko capitol hill akikabiliana na bunge jipya linalodhibitiwa na upinzani wa Republican akitoa wito wake wa kupandisha kodi kwa wamarekani matajiri.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:52 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Bwana Obama alianza mwaka wake wa saba kama kiongozi wa Marekani na akiwa amebakisha hotuba yake moja zaidi ya hali ya kitaifa. Ukusanyaji maoni wa umma unaonesha kuna wimbi jipya la umaarufu wakati uchumi wa Marekani ukiendelea kukua.

Wapiga kura wengi lakini sio wote wanaidhinisha hatua zake za karibuni za kurejesha uhusiano wa kawaida na Cuba na juhudi za kuruhusu wahamiaji wasio na vibali halali kubaki na kufanya kazi nchini marekani.

Rais Barack Obama
Rais Barack Obama

Kwa mara ya kwanza katika urais wake hata hivyo Rais huyo M-democrat anakabiliana na wa-Republican ambao wanadhibiti kote baraza la seneti na baraza la wawakilishi baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana.

Bwana Obama alitoa wito wa kupandisha kodi kwa faida za watu binafsi wanazopata katika mauzo ya mali kama hisa, bondi na kuondoa nafuu ya kodi kwa wauzaji nyumba za mamilioni ya dola na kuweka ada kwa makampuni makubwa ya fedha nchini Marekani. Rais anataka kutumia mapato yaliyokadiriwa dola bilioni 320 katika muda wa miaka 10 ijayo ili kutoa nafuu ya kodi kwa wamarekani wa kipato cha kati na kuondoa ada kwa wanafunzi wanaosoma vyuo vya kijamii.

Wakati bwana Obama alipokuwa akielezea baadhi ya mapendekezo yake katika siku za karibuni wa-Republican waliyashambulia vikali mapendekezo hayo na kusema yana gharama kubwa. Wabunge hao wa upinzani walisema ongezeko la kodi litazorotesha kuimarika kwa uchumi wa Marekani ulio mkubwa sana duniani.

Senata Joni Ernst, m-Republican
Senata Joni Ernst, m-Republican

Bunge halionekani kuunga mkono mpango wa kodi wa bwana Obama lakini kwa kutoa pendekezo hilo bwana Obama alionekana kufungua mjadala mkubwa nchini Marekani kuelekea kuelekea uchaguzi wa urais mwaka ujao ili apatikane mrithi wake.

Kwa upande wake bwana Obama anaapa kutumia kura ya turufu kwa idadi kadhaa ya vipaumbele vya Republican ikiwemo kuidhinisha uenzi wa bomba la mafuta lenye utata kutoka Canada kuelekea Marekani pamoja na mabadiliko ya kufuta mageuzi ya huduma ya afya na masharti ya kifedha huko Wall Street.

XS
SM
MD
LG