Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 18:02

Obama atowa wito kwa wafuasi wake kumchagua tena


Makamu Rais Joe Biden na Rais Barack Obama wakiwapungia wajumbe kwenye siku ya mwishoni mwa hotuba ya rais kwnye mkutano mkuu chama
Makamu Rais Joe Biden na Rais Barack Obama wakiwapungia wajumbe kwenye siku ya mwishoni mwa hotuba ya rais kwnye mkutano mkuu chama
Rais Barack Obama amekubali rasmi kuwa mgombea kiti cha rais kwa niaba ya chama cha Demokratik katika hotuba yake Alhamisi, aliyowahimiza wafuasi wake kuungana pamoja nae kaika awamu ya mwisho ya miezi miwili ya kampeni za kupigania kiti cha rais Marekani.

Ilikuwa hotuba yake muhimu kabisa kaika kampeni, na Wademoktrats walimpongeza kwa shangwa kubwa mjini Charlotte, alipotetea juhudi zake za kuokoa uchumi wa nchi hii, na kuwaomba wamrudhishe kwa awamu ya pili White House.

"Wamarekani na mtambuwe kitu kimoja, maatizo yetu yanaweza kutanzuliwa. Changamoto zetu zinaweza kutanzuliwa. Hivyo njia tunayopendekeza huwenda ikawa ngumu zaidi, lakini inatuongoza katika mahala bora zaidi. Na nina waomba muchaguwe mustakbal huo," alisema.

Bw. Obama alisema, uchaguzi wa mwaka huu kati yake na mgombea wa chama cha Republican Mit Romney, unawapatia Wamarekani chago la wazi kabisa katika kipindi cha kizazi kizima, juu ya uchumi, kodi, nishati, elimu na masuala ya amani na vita.
XS
SM
MD
LG