Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 03, 2022 Local time: 07:05

Obama atafuta uungaji mkono kushambulia Syria


Waandamanaji wakipinga hatua ya kijeshi dhidi ya Syria mjini New York
Utawala wa rais Obama unafanya msukumo mkali wa saa 48 ili kushawishi bunge na wananchi wa Marekani kuunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria.

Washauri wa ngazi ya juu wa kijeshi watafanya mikutano ya faragha na ya wazi na wabunge wiki hii. Rais atafanya mahojiano na mitandao mikubwa 6 ya televisheni leo Jumatatu kabla ya kutoa hotuba ya White House kwa taifa Jumanne usiku.

Utawala wa Obama pia unasambaza kanda za video kwa washirika wake, wabunge wa Marekani na mashirika ya utangazaji zikionyesha raia wa Syria ambao ni waathiriwa wa mashambulizi ya silaha za kemikali.

Maafisa wa Marekani wanasema wana ushahidi ambao unathibitisha pasipo shaka kwamba jeshi la Bashar Al Assad lilishambulia wapinzani wa serikali kwa gesi ya sumu katika maeneo ya Damascus mwezi uliopita na kuuwa zaidi ya watu 1,400.
XS
SM
MD
LG