Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Mei 31, 2023 Local time: 19:21

Obama asisitiza tena ushirikiano kati ya mataifa ya Kislamu na Magharibi


Rais Barack Obama akitoa hotuma katika chuo kikuu cha Indonesia mjini Jakatra hapo Novemba, 10 2010.

Rais Barack Obama wa Marekani ametoa wito wa ushirikiano na uhusiano mzuri kati ya waislamu na nchi za magharibi. Akitoa hotuba muhimu katika Chuo Kikuu cha Indonesia, mjini Jakatra Jumatano asubuhi, Bw Obama alisema, "Marekani haiko vitani na wala haitakua vitana na Uislamu."

Anasema anatambua haiwezekani kwa hotuba moja au mbili kufutilia mbali hali ya kutoaminiana iliyodumu kwa muda mrefu sana. Lakini alisema kama rais ameweka kipau mbele chake juhudi za kuanza kurekebisha ushirikiano huo ulozorota.

Rais Obama alitumia nafasi hiyo kuzungumzia masuala aliyozungumzia katika hotuba yake muhimu ya Cairo kwa Jumuia ya Kislamu duniani. Kuhusiana na Mashariki ya Kati aliahidi kuendelea na juhudi za kutafuta amani licha ya kile alichokieleza "vizingiti vikubwa".

Rais Obama alisifu demokrasia ya Indonesia na imani ya kustahmiliana kidini katika taifa lenye waislamu wengi duniani, akisema ni mfano wa kuigwa kote duniani.

Ziara hii yake ni ya kwanza huko Indonesia tangu alipoondoka miaka 1960, wakati aliishi huko pamoja na mamake alipokua mdogo kwa miaka minne. Na katika hotuba yake alisema anakumbuka maisha na ukarimu wa Indonesia akitaja baadhi ya maneno anayokumbuka.

Akiwa huko Jakatra, rais Obama na mweneyji wake Susilo Bambang Yudhoyono walitangaza makubaliano ya ushirikiano katika fani ya bisashara, elimu, nishati safi na usalama. Mapema Jumatano alitembelea mskiti wa Istiqal mjini Jakatra, ambao ni mkubwa kabisa huko Kusini Mashariki ya Asia.

Baada ya Indonesia rais Obama anaelekea Seoul, Korea ya Kusini kuhudhuria mkutano wa viongozi wa G-20, kabla ya kuhudhuria mkutano mwengine wa uchumi huko Japan.

XS
SM
MD
LG