Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:36

Obama asema kuzuia Ebola ni jukumu la wote


Baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi yaliokumbwa vibaya na Ebola, August 30, 2014
Baadhi ya mataifa ya Afrika magharibi yaliokumbwa vibaya na Ebola, August 30, 2014

Rais wa Marekani Barack Obama anasema jumuiya ya kimataifa inahitaji kuchukua hatua kuhusu mgogoro wa ugonjwa wa Ebola ulioibuka katika mataifa kadhaa ya Afrika magharibi mahala ambako anasema ukosefu wa miundo mbinu ya huduma za afya imepelekea kusambaa kwa “tatizo ambalo linazuilika.”

Bwana Obama alikiambia kituo cha televisheni cha NBC cha nchini Marekani kwamba uwezo wa jeshi la Marekani unahitajika kuweka vituo vilivyotengwa pamoja na vifaa na kutoa usalama kwa wafanyakazi wa afya wa kimataifa. “Kama hatutafanya juhudi hizo hivi sasa na kusambaa kwa ugonjwa huu sio tu kwa bara la Afrika lakini hata sehemu nyingine za dunia kuna uwezekano wa virusi hivyo kugeuka geuka na inakuwa rahisi sana kuambukiza wengine”.

Bwana Obama alisema anaamini kwamba Marekani inahitajika kuweka mpangilio wa kukabiliana na mlipuko wa Ebola kama kipaumbele cha usalama wa kitaifa.

Mlipuko wa Ebola umeshauwa zaidi ya watu 2,000 hasa katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Wakati huo huo Waziri wa Ulinzi wa Liberia, Brownie Samukai aliiambia Sauti ya Amerika-VOA kwamba nchi yake inafurahia msaada wowote utakaopatikana kutoka Marekani akisema uchumi wa Liberia umesimama kwa sasa na hiyo ni changamoto kubwa inayochochea kutoweza kutoa huduma za msingi za afya.

Nkosazana Dlamini-Zuma
Nkosazana Dlamini-Zuma

Naye mwenyekiti wa Umoja wa Afrika-AU, Dlamini-Zuma alielezea umuhimu wa elimu ya afya kwa umma na juhudi ambazo hazikumbatii unyanyapaa na kutengwa kwa wagonjwa.

Utafiti mpya unaonyesha kuwa majaribio ya chanjo ya Ebola ambayo imefanyiwa kwa tumbili yanaweza kufanya kazi kwa wiki tano au hadi miezi 10 kama ikitumiwa kikamilifu.

XS
SM
MD
LG