Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 26, 2023 Local time: 06:12

Obama apongeza uchaguzi wa Nigeria


Rais anayeondoka madrakani Goodluck Jonathan, na rais aliyeshinda uchaguzi nchini Nigeria Muhammadu Buhari

Muhammadu Buhari aapa kuliangamiza kundi la Boko Haram

Rais wa marekani, Barack Obama amewasihi wote mshindi na kadhalika aliyeshindwa kwenye uchaguzi, kwa kufanya kazi pamoja katika kuunganisha taifa hilo la Nigeria.

Jumatano, Bw.Obama alimpigia simu rais aliyechaguliwa Muahhamadu Buhari pamoja na aliyekuwa rais hapo awali, Goodluck Jonathan. Aliwapongeza wote wawili, Bw. Buhari kwa ushindi wake na Bw Jonathan kwa kukubali matokeo ya uchaguzi huo. Bw. Obama alisema kwamba Marekani itaendelea kuisaidia Nigeria inapokabiliana na changamoto mbali mbali kama vile tishio kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram. Mapema jana, Bw Buhari aliapa kwamba serikali yake itafanya kila iwezalo kuliangamiza kundi la Boko Haram.

XS
SM
MD
LG