Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 02, 2023 Local time: 05:16

Obama amtuza shujaa wa kijeshi.


Rais Obama wa Marekani akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya siku kuu ya kuwakumbuka wanajeshi waliohudumu.

Rais wa marekani Barack Obama ametoa medali ya heshima kwa kapteni wa jeshi aliekabiliana na mshambuliaji wa kujitoa mhanga aliekuwa karibu kujilipua Afghanistan 2012 huku akijiokoa pamoja na wenzake wengi.

Obama alimvisha medali hiyo kwenye shingo kapteni mstaafu Florent Groberg Alhamisi kwenye hafla iliofanyika katika ikulu ya White House akisema kuwa afisa huyo alionyesha ujasiri mkuu.

Hata hivyo, wanajeshi watatu na mfanyakazi mmoja wa kigeni waliuwawa kwenye shambulizi hilo huku Groberg akipata jeraha baya kwenye mguu lililopelekea upasuaji mara 33 ili kuuokoa.

Groberg mwenye umri wa miaka 32 aliuguza majeraha kwa miaka 3 katika hospitali ya kijeshi , na sasa amestaafishwa kwa sababu za kiafya. Groberg ndie mwanajeshi wa 10 wa marekani kutambuliwa kwa jukumu lake kwenye mapigano nchini Iraq na Afghanistan. Medali ya heshima ndio ya juu zaidi marekani inayoashiria ujasiri kwenye vita.

XS
SM
MD
LG