Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 14:34

Obama Amsisitiza Kagame kutowasaidia M23


Rais wa Marekani Barack Obama
Rais wa Marekani Barack Obama amemsisitiza Rais wa Rwanda Paul Kagame umuhimu wa kusitisha kabisa uungaji mkono wowote kwa waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

Jopo moja la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linaishutumu Rwanda na Uganda kwa kuliunga mkono kundi la uasi la M23 ambalo karibuni liliondoka kutoka Goma baada ya kuuteka mji huo wa mashariki mwa Congo. Wote Rwanda na Uganda wanakanusha madai hayo.

White House inasema Obama alimsihi Kagame wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu Jumanne kutekeleza kikamilifu ahadi zake alizotoa katika mazungumzo ya amani ya kieneo juu ya kubuni makubaliano ya kisiasa ambayo yanajumuisha kumalizika uepukaji wa sheria kwa makamanda wa M23 ambao wametenda ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Anasema mzozo huo ni budi umalizike kwa makubaliano ambayo yatalinda hadhi ya kitaifa ya DRC na kuzungumzia usalama wa kieneo pamoja na masuala ya uchumi na utawala.

Wakati huo huo wizara ya fedha nchini Marekani ilitoa vikwazo vipya Jumanne dhidi ya viongozi wawili waandamizi wa kundi la M23 kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na harakati nyingine zinazochangia mapigano nchini DRC.

Inasema Baudoin Ngaruye na Innocent Kaine wanahusika kwa vitendo vibaya vya ghasia na kwamba Kaine alifanya vitendo vinavyowalenga watoto kupitia mauaji, ukataji viungo vya mwili na ghasia za ngono.

Pia Jumanne wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walisema ushahidi wa awali kuhusu mashitaka ya shutuma za ghasia zilizotokea mwezi uliopita huko Minova karibu na Goma zilionesha kesi 126 zilizoripotiwa za ubakaji na mauaji ya watu wawili.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema uchunguzi tofauti uliofanywa na jeshi la Congo umepelekea kukamatwa kwa wanajeshi tisa wakiwemo wawili wakihusika na ubakaji na saba wengine walihusishwa na wizi wa ngawira.

Ripoti kamili ya Umoja wa Mataifa juu ya shutuma za ukiukwaji inatarajiwa kutolewa mwezi Januari mwakani.
XS
SM
MD
LG