Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 05:27

Obama amewasihi wahitimu kufanikisha mabadiliko ya matumaini duniani


Rais Barack Obama akiwa katika mahafali ya chuo kikuu cha Rutgers, May 15, 2016.

Rais Barack Obama aliwasihi wahitimu kwenye chuo kikuu cha Rutgers nchini Marekani kufanikisha mabadiliko chanya katika dunia licha ya changamoto zilizopo.

Viongozi kwenye chuo kikuu cha New Jersey huko Marekani walimshawishi bwana Obama kwa miaka kadhaa kuhutubia kwenye mahafali ya 250 ya shule hiyo. Inatambulika kuwa heshima kubwa kwa shule au chuo kumwalika rais aliyeko madarakani au wa zamani kuzungumza kwenye mahafali.

Rutgers ni chuo kikuu cha umma ambacho White House inakisifia kama taasisi inayotambulika kwa kujiendeleza zaidi kimasomo. Msemaji wa White House, Josh Earnest alisema hotuba ya bwana Obama aliyoitoa Jumapili ilikuwa na mtazamo kuhusu dunia ambapo darasa la mwaka 2016 linajiandaa kuingia huko.

Pia msemaji huyo alisema bwana Obama anaamini kwamba wanafunzi wa chuo kikuu cha Rutgers wamejiandaa vilivyo kama wanafunzi wengine waliohitimu kukabiliana na changamoto hizo na kutumia mabadiliko haya ya mazingira kuunda dunia bora zaidi.

XS
SM
MD
LG