Rais Barack Obama anasema kikosi hicho cha hadi wanajeshi 275 kimeanza kuwasili na kutoa msaada na ulinzi wa wafanyakazi wa marekani na ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.
Siku ya Ijuma rais alisema hatowarudisha wanajeshi wa Marekani katika mapambano huko Iraq. Lakini katika barua yake kwa bunge siku ya Jumatatu, alidokeza kwamba wanajeshi wanaokwenda Iraq hivi sasa wanabeba silaha na wako tayari kwa mapigano ikihitajika.
Bw Obama alikutana na washauri wake wa usalama wa kitaifa Jumatatu jioni baada ya kurudi kutoka ziara ya miwshoni mwa wiki katika jimbo la California. Washauri hao wamekua wakifanya kazi ili kumtayarishia orodha ya mapendekezo ili kukabiliana na uwasi wa wasuni ambao umefanikiwa kuchukua udhibiti wa sehemu kubwa ya kaskazini ya Irak na kutishia kuishambulia Baghdad.
Iran ambayo si mshirika wa Marekani imeeleza pia wasi wasi kuhusiana na ghasia za Irak na katika hatua isiyo ya kawaida Jumatatu, maafisa wa Marekani walizungumza na wale wa Iran juu ya uwezekano wa kushirikiana, kando ya mazungumzo ya nuklia mjini Vienna.
Akizungumza kwenye ndege ya Rais Obama walipokua wanarudi Washington msemaji wa White House Josh Earnest alipinga uwezekano wowote wa ushirikiano wa kijeshi na Iran
“Mazungumzo yeyote na utawala wa Iran hautohusu uratibu wa kijeshi hatuna hamu na juhudi zezote za kuratibu shughuli za kijeshi na Iran.”
Maafisa wa Marekani wanasema wanajeshi 170 tayari wako Irak na wengine 100 huwenda wakapelekwa wakihitajika.
Maafisa wanasema wanajeshi wanaingia Irak kwa idhini kutoka serikali ya Irak na watasaidia katika kuwahamisha baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi wa Marekani mjini Baghdad. Ubalozi unaendelea kufanya kazi.
Serikali ya Marekani ilijaribu kuwahakikishia wamarekani Jumatatu kwamba kupelekwa kwa wanajeshi haitomaanisha kuanzishwa tena kupelekwa wanajeshi Irak bila ya muda maalum. Katika barua yake rais Obama ameliambia bunge kwamba wanajeshi watabaki huko hadi usalama unarudi kuwa shuwari tena na hawatohitajika huko.
Na katika uwanja wa mapigano wanamgambo wa kisuni waliuchukua mji wa Telafar Jumatatu, lakini waziri mkuu na msemaji wake wanaendelea kusisitiza kwamba majeshi ya serikali yanapata ushindi.
Mataifa mengi yameanza kuwaamrisha wafanyakazi wao kuondoka kutoka Baghdad wakati wasi wasi unaongezeka kutokana na uwezekano wa mashambulio kuwasili Baghdad karibuni.