Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:04

Rais Barack Obama akutana na rais mteule wa Marekani Donald Trump

Rais Barack Obama amekutana na rais mteule Donald Trump
Rais Barack Obama amekutana na rais mteule Donald Trump

Rais Obama ameagiza idara za serikali kushirikiana vyema katika kipindi cha mpito wa kubadilishana madaraka rasmi kuelekea kuapishwa kwa rais mteule Januari 20 mwaka 2017.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amekutana na rais Barack Obama Ikulu ya White House katika ziara yake ya kwanza kwa mazungumzo na Rais wa Marekani anayemaliza muda wake.

Rais Obama ameagiza idara za serikali kushirikiana vyema katika kipindi cha mpito wa kubadilishana madaraka rasmi kuelekea kuapishwa kwa rais mteule Januari 20 mwaka 2017.

Kabla ya mkutano huo ikulu ya Marekani ilisema Makabidhiano ya madaraka kwa Amani ni kanuni ya demokrasia ya nchi.

Mke wa Rais Obama, Michelle Obama naopia alikutana faragha na mke wa Trump, Melania Trump, wakizungumzia kuhusu maisha ya kila siku ndani ya jengo hilo la White House.

Inaelezwa kwamba maafisa wa Obama wanahakikisha kuwa Trump na maafisa wake wakuu ambao bado hawajatajwa wanaandaliwa kutoka siku ya kwanza ili kulinda usalama wa taifa la Marekani.

Maafisa wa ujasusi na usalama wanaanza kumweleza Trump habari za kila siku juu ya vitisho vinavyohusiana na usalama wa nchi na operesheni za jeshi la Marekani nje ya nchi.

XS
SM
MD
LG