Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 28, 2024 Local time: 15:16

Obama aanza mikutano Korea Kusini


Rais Obama akikagua gwaride baada ya kutua Seoul, Korea Kusini.
Rais Obama akikagua gwaride baada ya kutua Seoul, Korea Kusini.

Rais Obama ameanza kukutana na viongozi mbali mbali huko Korea Kusini kabla ya mkutano wa G20.

Rais Barack Obama wa Marekani amewasili Korea Kusini ambako atakuwa na mikutano na mwenzake wa nchi hiyo na viongozi wengine mbali mbali kabla ya kuanza kwa mkutano wa nchi za G20 hapo Alhamisi.

Bwana Obama anakabiliwa na siku za majadiliano magumu huko. Majadiliano miongoni mwa wasaidizi wanaoandaa taarifa ya mkutano huo yamekuwa magumu, kulingana na maafisa wa serikali ya Korea Kusini, wenyeji wa mkutano. Kundi hilo la G20 linakabiliwa na tofauti ndani yake kuhusu namna ya kushughulikia uwiano wa biashara na viwango vya ubadilishaji fedha.

Kabla ya kuwasili Korea Kusini Rais Obama alikuwa Jakarta ambako alisifu kundi la G20 kuwa na mahali muafaka kujadili maswala ya uchumi wa dunia.

XS
SM
MD
LG