Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 26, 2020 Local time: 10:01

Obama aahidi kutembelea Kenya

Rais wa Marekani Barack Obama

Shirika la utangazaji la Kenya – KBC - linaripoti kwamba Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuitembelea nchi hiyo mahali alipozaliwa baba yake kabla hajaondoka madarakani.

Shirika la utangazaji la Kenya – KBC - linaripoti kwamba Rais wa Marekani Barack Obama ameahidi kuitembelea nchi hiyo mahali alipozaliwa baba yake kabla hajaondoka madarakani.

KBC imesema bwana Obama alitoa matamshi hayo katika mahojiano maalum yaliyofanyika Juni mosi hapa Washington. Bwana Obama ameshaitembelea Kenya mara tatu, lakini hajawahi kwenda tangu awe Rais.

Bwana Obama alimjua kidogo tu baba yake, ambaye alifariki katika ajali ya gari mwaka 1982. Hata hivyo, wakenya walifuatilia kwa karibu uchaguzi wa Barack Obama kama Rais na wengi wanamchukulia kama ni mwenzao.

Makamu Rais wa Marekani Joe Biden anatarajiwa kuitembelea Kenya wiki ijayo katika ziara ya mataifa matatu ambayo itamfikisha pia Misri na Afrika Kusini.

Kura ya Maoni : Uchaguzi Tanzania

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

Kama unapiga kura leo utampigia nani kura yako ya urais?

Kura hii ya maoni si ya kisayansi na inaonyesha maoni ya waliojibu maswali tu.

XS
SM
MD
LG