Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 27, 2024 Local time: 04:30

Obama aagiza majeshi ya Marekani kumsaka Joseph Kony


Rais Barack Obama.
Rais Barack Obama.

Majeshi ya Marekani yatashirikiana na wanajeshi wengine walioko Afrika ya kati kumsaka Joseph Kony .

Rais wa Marekani Barack Obama anapeleka kikosi cha wanajeshi wapatao 100 wa Marekani kusaidia kumsaka kiongozi wa kundi la waasi la Lords Resistance Army nchini Uganda.

“Nimetoa agizo kwa kikosi kidogo cha wanajeshi wa nchi kavu kwenda Afrika ya Kati ili kusaidia majeshi ya kanda hiyo kumwondoa Joseph Kony kutoka kwenye uwanja wa mapambano”. Obama alisema hayo kwenye barua yake kwa spika wa bunge John Boehner na Daniel Inouye rais wa baraza la seneti .

“Ninaamini kupeleka majeshi haya ya Marekani ni kutekeleza zaidi matakwa ya usalama wa taifa la Marekani na sera za nje na itakuwa ni mchango mkubwa katika juhudi za kupambana na LRA huko Afrika ya Kati”.

Obama aliongeza kwamba kundi hilo limeuwa , kuteka nyara maelfu ya watu wanaume , wanawake na watoto huko Afrika ya Kati. Na kuendelea kufanya unyama kwenye Jamhuri ya Afrika ya Kati, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudan Kusini na zina athari isiyo sawa kwenye usalama wa kanda hiyo”.

Amesema Marekani imeunga mkono juhudi za kijeshi kwenye kanda hiyo tangu mwaka 2008 kuwasaka Lord’s Resistance Army lakini hawakufanikiwa. Wanajeshi wa Marekani watasaidia majeshi yaliyoko kwenye kanda hiyo ambayo yanafanya kazi kumsaka Joseph Kony na viongozi wengine wa juu wa kundi hilo. Rais amesema majeshi yake hayatapambana na Joseph Kony isipokuwa tu ikibidi kwa kujilinda.

XS
SM
MD
LG