Mgogoro unao karibia kufikia miaka miwili wa Ethiopia, umesababisha takriban nusu ya watu wote katika taifa hilo kutokuwa na chakula cha uhakika.
Pia, makundi ya misaada yanataabika kufika katika maeneo ya vijijini kwa sababu ya kutokuwepo mafuta ya kutosha shirika la mpango wa chakula duniani (WFP) limesema Ijumaa.
Licha ya kwamba usambazaji wa misaada ulianza baada ya serekali kuu kutangaza kusimamishwa kwa mapigano na pande zote mwezi Machi, kiwango cha utapia mlo kimeongezeka na kinatarajiwa kuwa kibaya zaidi limesema shirika hilo la Umoja wa Mataifa baada ya kufanya tathimini yake.
Shughuli kama vile za kibenki na mawasiliano zimesimamishwa katika mkoa wa Tigray, ambao una jumla ya watu milioni 5.5, siku kadhaa baada ya jeshi na vikosi vya ushirika kujiondoa katika eneo hilo.
Huduma hizo bado hazijarudishwa na kusababisha mazingira magumu kwa watu kununua chakula.