Waziri Mkuu wa Norway amependekeza leo Jumatatu msaada wa dola bilioni 7.3 kwa Ukraine ikiwa ni uungwaji mkono wa karibuni kutoka kwa washirika wa Ukraine wa Ulaya wakati ikipambana na uvamizi wa Russia.
Waziri Mkuu Jonas Gahr Stoere aliwaambia waandishi wa habari baada ya kukutana na viongozi wa upinzani kwamba msaada huo utatolewa kwa kipindi cha miaka mitano na kwamba serikali yake inataka kuongeza msaada zaidi kwa nchi nyingine zilizoathiriwa na mzozo huo.
"Tunapendekeza kwamba Norway itoe mchango wa kisheria na wa kudumu kwa Ukraine," alisema.
Bunge la Norway lazima liidhinishe msaada huo.
Gazeti la Financial Times liliripoti Jumatatu kwamba Umoja wa Ulaya unajiandaa kwa ziara inayowezekana kufanywa wiki hii na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy kulihutubia Bunge la Ulaya.
Facebook Forum