Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:24

Njama za kumuuwa Rais wa Benin zafichuka


Rais wa Benin Boni Yayi
Rais wa Benin Boni Yayi
Watu watatu wameshtakiwa kwa njama za kutaka kumpa sumu Rais wa Benin Thomas Boni Yayi akiwemo mpwa wake na daktari wake binafsi.

Wendesha mashtaka wanasema mpwa wa rais huyo Zouberath Kora na daktari wa rais huyo Ibrahim Mama Cisse walikuwa wameahidiwa hadi dola milioni 2 kwa jukumu lao katika njama hizo. Watuhumiwa hao wawili yaripotiwa walitakiwa kuchanganya dawa za Rais Boni Yayi na sumu wakati akiwa ziarani mjini Brussels, Ubelgiji.

Njama hizo yadaiwa zilipangwa na Patrice Talon mfanyabiashara wa Benin ambaye katika siku za karibuni amekuwa na mzozo na rais huyo. Maafisa wanamsaka bwana Talon ambaye hivi sasa yuko nje ya nchi. Wapelelezi wanasema njama hizo zilifichuka baada ya mpwa wa Rais Boni kumwelezea mtu mwingine kwenye jamii ya rais huyo juu ya njama hizo.

Wote Kora na Dr. Cisse pamoja na waziri wa zamani wa biashara Maoudjaidou Soumanou wamekamatwa na kushtakiwa kwa jaribio la mauaji na njama za kutaka kumwua rais huyo. Bwana Boni Yayi aliingia madarakani nchini Benin mwaka wa 2006. Mwaka wa 2007 alinusurika shambulizi la bunduki baada ya msafara wake kushambuliwa. Alishinda tena kiti cha urais mwaka jana.
XS
SM
MD
LG