“Nilikuwa ni kijana mweusi ambaye hakutaka kuwa mweusi. …Watu weusi walikuwa wanatisha,” anaeleza umma uliohudhuria onyesho lake, kwa kicheko chenye wasiwasi.
Na baada ya muda fulani, ameingiwa na hisia za upweke – siyo tu kuburudisha, lakini pia kuwasiliana na familia zinazolea watoto wa rangi tofauti ambao anawafundisha. Lengo : anawasaidia wanaolelewa kujenga uelewa bora wa utambulisho wao wakati wakipita katika tabaka za rangi.
Akiwa katika umri wa miaka 40, Goller-Mpita njia alichukuliwa kulelewa akiwa na umri wa miezi 13 na familia ya wazungu wanaoishi Takoma, Kaskazini magharibi ya Jimbo la Washington, Marekani. Nilipokuwa nao nilikuwa nashiriki kama mtoto wa kizungu. Hapakuwa na mtu mweusi katika mazingira yangu.
Anasema wazazi wake “walifanya mengi” kumshirikisha yeye, na pia kaka yake na dada yake, ambao ni weusi.
“Tulihamia Afrika kwa miaka kadhaa. Tuliporejea Marekani wazazi wangu walitupeleka katika shule iliyokuwa na watu weusi, lakini hiyo haikuvunja ari ya kuwa mzungu.
Goller-Mpita Njia anasisitiza kuwa wazazi wake katika familia za mchanganyiko wa rangi “wanajukumu kumuandaa mtoto wao siyo kukabiliana na ulimwengu wanaoishi, lakini muhimu zaidi, katika dunia watakayo ishi mpaka kufikia uzee wao.”
Alitambua kuwa wakati alipata kujua fursa za kuishi katika maeneo ya wazungu akiwa kijana, anaweza kuangaliwa kama ni tishio katika mazingira hayo hayo kama mtu mzima mweusi.
Anaibua maudhui hayo katika moja ya maonyesho yake akiwa peke yake, katika historia ya maisha yake Riding in Cars With Black People & Other Newly Dangerous Acts.” “akipanda magair akiwa na watu weusi na mambo mapya mengine yaliyohatarishi.” Onyesho jingine, “Sitting in Circles With Rich White Girls: Memoirs of a Bulimic Black Boy," anagundua juhudi zake za kukubalika katika jamii hiyo.
Ili kuwasaidia wanaolelewa uhimilivu, pia anawataka wazazi wao kujenga au kuweka mafungamano kati ya mtoto huyo na familia aliyozaliwa nayo.
“Watu wengi wanasahau kuwa wanaolelewa wanasimulizi kabla hawajaja kuungana na wewe, hata pale wanapozaliwa,” amesema Goller-Sojourner, ambaye aliongeza katika jina la familia wakati akiwa mtu mzima ili kukidhi tabia y udadisi aliyokuwa nayo.
Historia yake ya huko nyuma ilijitokeza kuwa wazi zaidi miaka michache iliyopita, wakati alipokuwa anaweza kumfuatilia ndugu wa kike wa mama yake mzazi. Alimtumiapicha za mama yake mzazi, Yolandia-Maria Hurtt, muigizaji ambaye alikuwa eneo la Broadway, na pia katika jimbo la Midwestern huko Ohio. Alifariki mwaka 2011.
Albamu hilo lenye picha linampa fursa Goller-Sojourner mafungamano ya upendo halisia na Hurtt.
“Hii ni kazi yake. Athari zake ziko hapa. Athari zangu ziko hapa. Pamoja na kuwa amekufa, ninamgusa mama yangu – siyo kwa hisia, lakini kwa uhakika. Na hilo bila shaka ni kitu kiko nje ya lile niliowahi kulifikiria linawezekana.