Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 15:57

Makubaliano baina ya waasi wa Avengers wa eneo la Niger Delta na serikali ya Nigeria yatetereka


Waasi katika eneo la Niger Delta, Nigeria
Waasi katika eneo la Niger Delta, Nigeria

Serikali ya Nigeria ina hari kubwa ya kupata suluhisho kwa miezi ya mashambulizi kwenye miundo mbinu yake muhimu katika eneo la Niger Delta, lakini makubaliano ya kusitisha mapigano yaliotangazwa na maafisa Jumanne yanaonekana kutetereka.

Afisa mkuu wa shirika la mafuta linalomilikiwa na serikali, ambaye hakutaka kutajwa jina , aliithibitishia voa kuhusu makubaliano ya kusitisha mapambano , lakini hakutowa maelezo zaidi.

Kundi la wanamgambo la Niger Delta, Avengers lilisema kwenye mtandao wa twitter, hakuna usitishaji wa mapigano uliofikiwa.

Miezi ya mashambulizi ya kundi la Avengers kwenye miundo mbinu ya petrol katika Delta yamepelea kushuka kwa uzalishaji wa mafuta wa Nigeria kwa takriban nusu kiwango cha kawaida cha mapipa millioni 2 kwa siku.

Mafuta ndio bidhaa kubwa ya Nigeria inayosafirisha nje. Wachambuzi wametaja kushuka kwa uzalishaji kama mojawapo ya sababu uchumi wa taifa hilo ambao ni mkubwa Zaidi barani Afrika karibuni utadorora.

Mapema mwezi hu serikali ilitangaza kuwa inasitisha operesheni za kijeshi katika eneo la Delta ili kufungua njia kwa majadiliano.

Naibu waoperesheni kwa Afrika katika shirika la kijasusi la Stratfor, Mark Schroeder, anasema usitishaji wa mapigano huwenda ikawa mbinu ya uchelewesho wa rais Muhammadu Buhari.

Bw. Shchroeder anasema, huwenda ikawa ni mbinu ya rais Buhari anahitaji kujadiliana au kupanga na majimbo mengine ya kisiasa iwapo anaweza kuongeza ushirikiano wa mapato na eneo la Niger delta

Eneo la kusini la Delta ni makazi ya takriabn uzalishaji wote wa mafuta Nigeria, lakini bado linabaki kuwa eneo lenye umasikini. Uasi sio jambo jipya huko. Waasi kama hao waliibuka mwaka 2009, pale serikali ilipoanza kuwalipa wapiganaji na kuwapatia mafunzo ya ajira kwa mbadala wa kusitisha mapigano.

The Avengers, kundi lisilojulikana ambalo huwasiliana kupitia mtandao wa Twitter, halikuweza kupatikana kutowa maoni yao.

Katika taarifa wiki ilopita The Avengers waliitaka serikali kujitahidi kufanya mazungumzo na wapatanishi huru.

Mgogoro juu ya kuwepo kwa usitishaji wa mapigano huwenda ikawa ishara ya mgawaniko ndani ya kundi la The Avengers, alisema Bw. Schroeder. Au inaweza kuwa tu ni ukosefu wa mustahmala na serikali ya Buhari. Mengi yay ale kundi hilo linadai ni masuluhisho kwa uteshi wa mda mrefu wa Delta.

Bw Schroeder anasema, kile wanachotaka kuona kuliko yote, ni pendekezo la nia ya dhati kutoka kwa serikali ya Buhari.

Shambulizi la hivi karibuni la Avengers lilitokea hapo June 16 .

XS
SM
MD
LG