Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 07, 2023 Local time: 01:02

Nigeria yapunguza bei ya mafuta baada ya mgomo na maandamano


Vijana wenye hasira wakipiga makelele mjini Lagos dhidi ya bei za juu za mafuta

Serikali ya Nigeria imepunguza bei ya mafuta katika juhudi za kuridhisha wananchi, baada ya mgomo wa wiki moja na maandamano ambyo mara kadhaa yaligeuka na kuwa ghasia.

Katika hotuba yake kwa taifa Jumatatu, Rais Goodluck Jonathan amesema kwamba sasa bei itakuwa senti 60 kwa lita, hiyo ikipunguka kwa takriban asilimia 35.

"Serikali itaendelea kushinikiza kuwepo na mfumo wa masoko huru katika sekta ya mafuta. Ingawa tunaona jinsi maisha yalivyo magumu kwa wa Nigeria na baada ya kutafakari na mashauriano kati ya utawala na uongozi wa bunge, serikali imeidhinisha kupunguza bei ya mafuta inayouziwa raia na kua naira 97 kwa lita."

Kufuatia uwamuzi huo viongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Nigeria wamesema watahirisha mgomo wa kitaifa wa kupinga bei ya mafuta ambao umedumaza uchumi wa nchi hiyo kwa wiki nzima..

Bei ya mafuta inaendelea kuwa juu zaidi ya asilimia 45 kwa lita ambayo wa Nigeria wamelipa kabla yay a serikali kusitisha ruzuku maarufu ya mafuta siku ya mwaka mpya. Ruzuku hiyo ilikuwa moja ya mafao machache ambayo watu wa Nigeria wanafurahia kutoka taifa hilo lenye utajiri wa mafuta.

Kuondolewa Ruzuku hiyo kulisababisha bei ya mafuta ya taa kuongezeka mara mbili dufu kutoka dola 1.70 za Marekani kwa galoni au centi 45 kwa lita na kuwa dola 3.50 kwa galoni au senti 94 kwa lita.

Maelfu ya watu, wengi wakiwa wanaishi chini ya dola mbili kwa siku walianza maandamano katika miji mbali mbali kueleza kutoridhika kwao na kupanda kwa bei ya usafiri na chakula.

XS
SM
MD
LG