Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Februari 08, 2023 Local time: 23:54

Ngeria yamkamata mshukiwa wa mabomu.

kikosi cha jeshi Nigeria

Jeshi limetoa tangazo hilo Alhamisi jioni. Msemaji wa jeshi kanali Sani Usman amesema ukamataji huo umefanyika kwenye kituo kimoja cha ukaguzi cha jimbo la Gombe, ikiwa ni majibu ya kutolewa motisha.

Jeshi la Nigeria linasema limemkamata mshukiwa anayeaminika kuwa mpangaji mkuu wa mabomu ambayo yaliuwa Zaidi ya watu 70 katika miji ya Jos na Zaria wiki hii.

Jeshi limetoa tangazo hilo Alhamisi jioni. Msemaji wa jeshi kanali Sani Usman amesema ukamataji huo umefanyika kwenye kituo kimoja cha ukaguzi cha jimbo la Gombe, ikiwa ni majibu ya kutolewa motisha.

Amesema mshukiwa ambaye hakutajwa jina alikamatwa pamoja na watu wengine.

Usman amesema ukamataji huo ulikuwa ni operesheni mchanganyiko kati ya wizara ya mambo ya ndani nchini humo na vikosi vya serikali.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika kwa mashambulizi hayo, lakini yamekuja wakati wa mfululizo wa ghasia zilizodaiwa kufanywa na kundi la Boko haram ambalo limesababisha Zaidi ya vifo vya watu 200 katika wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG