Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 05, 2024 Local time: 15:18
VOA Direct Packages

Nigeria yaidhinisha chanjo ya Malaria ya Oxford siku chache baada ya Ghana


Picha ya mtoto akipewa chanjo ya Malaria
Picha ya mtoto akipewa chanjo ya Malaria

Idara ya taifa ya kuratibu dawa ya Nigeria Jumatatu imeidhinisha chanjo ya Malaria iliyotengezwa na chuo kikuu cha Oxford, ikiwa nchi ya pili kuchukua hatua hiyo baada ya Ghana iliyofanya hivyo wiki iliyopita.

Hata hivyo hatua hiyo inasemekana kuwa isiyo ya kawaida kutokana na kuwa imetangazwa kabla ya kumalizika kwa awamu ya mwisho ya majaribio ya chanjo hiyo. Idara hiyo ya Nigeria inayosimamia ubora wa chakula na dawa, maarufu NAFDAC, imesema kwamba chanjo hiyo ya R21 ya Malaria itatumika kwa kufuata maagizo ya shirika la afya duniani WHO.

Ugonjwa wa Malaria unaosababishwa na mbu huuwa zaidi ya watu 600,000 kila mwaka, wengi wao wakiwa ni watoto wachang na wadogo barani Afrika. Nigeria ambayo ina idadi kubwa sana ya watu barani humo ndiyo iliyoathiriwa zaidi na Malaria, ikiwa na asilimia 27 za maambukizi na asilimia 32 ya vifo kutokana na Malaria ulimwenguni, kwa mujibu wa ripoti ya WHO ya 2021.

Haijabainishwa ni lini chanjo hiyo itakapoanza kutumika Nigeria na Ghana, kwa kuwa WHO inaendelea kutathmini matumizi pamoja na usalama wake.

XS
SM
MD
LG