Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:11

Rais wa Nigeria ateuwa mawaziri


Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, mwenye kofia nyeusi (kati) akizungumza na waandishi wa habari huko Abuja nchini Nigeria
Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, mwenye kofia nyeusi (kati) akizungumza na waandishi wa habari huko Abuja nchini Nigeria

Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria amewasilisha orodha yenye majina 34 ya wajumbe wa baraza la mawaziri bungeni kupata uthibitisho.

Rais wa Seneti David Mark alisoma orodha hiyo ambayo haikuwa na maelezo ya wizara watakazoongoza kwa bunge Jumanne.

Baadhi ya mawaziri waliopendekezwa ni pamoja na aziri wa zamani wa fedha, Olusegun Aganga, mkurugenzi wa zamani wa kampuni ya Goldman Sachs. Waziri wa zamani wa mafuta Deziani Alison-Madueke pia yupo kwenye orodha.

Vyanzo vya serikali vinasema kuna ripoti kwamba Rais Jonathan amezungumza na mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Dunia, Ngozi Okonjo-Iweala kuhusu uwezekano wa kurudi kwake serikalini, japokuwa jina lake halikuwemo kwenye orodha iliyowasilishwa Jumanne.

Okonjo-Iweala alihudumu kama waziri wa fedha chini ya Rais wa zamani wa Nigeria, Olesegun Obasanjo.

Vyanzo vya serikali vinasema mazungumzo yanaendelea na kwamba anataka madaraka makubwa kuliko nafasi aliyokuwa nayo awali ya waziri wa fedha.
Orodha ya baraza la mawaziri ni hatua ya kwanza ya uteuzi wa bwana Jonathan tangu alipoapishwa kushika madaraka kwa muhula wa kwanza kama Rais mwezi uliopita.

XS
SM
MD
LG