Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 02:52

Nigeria kuanza kutoa vibali kwa watu kubeba bunduki.


Nigeria Attack

Jimbo la Zamfara nchini Nigeria litaanza kutoa vibali kwa ajili ya watu kubeba bunduki kujijitea wenyewe dhidi ya makundi ya utekaji yenye silaha yanayofanya uhalifu kaskazini magharibi mwa nchi, kamishna wa mawasiliano amesema Jumapili.

Makundi yenye silaha kaskazini magharibi mwa Nigeria yameongezeka wanavamia na kuteka watu na kudai malipo ya fidia, na ghasia zimekuwa kwa hali ya juu sana huku vikosi vya usalama vikishindwa kuzuiya mashambulizi hayo.

Watu wenye silaha wanafanya operesheni zao katika maeneo ya mbali ya misitu kaskazini magharibi mwa nchi na mashambulizi yao yenye mauaji yanalenga wanavijiji , wakulima, na wasafiri .

Shirika la habari la Reuters linaripoti kwamba mashambulizi hayo yameongezeka zaidi ya mwanzoni mwa mwaka huu.

Jimbo la Zamfara na eneo jirani la Kaduna yamepigwa vibaya na mashambulizi hayo, maafisa wameeleza.

Ibrahim Magaji Dosara ni kamishna wa habari huko Zamfara anasema gavana wa serikali ameamuru jeshi la polisi litoe vibali vya silaha 500 katika majimbo 19 kwa wale wanaotaka kujitetea wenyewe.

Ili kumiliki silaha katika jimbo la Zamfara unahitaji kuwa na kibali kutoka kwa gavana na kamishana wa polisi.

Vikosi vya usalama nchini Nigeria vinapambana na wanamgambo wa kiislamu wenye msimamo mkali kaskazinimashariki mwa nchi .

XS
SM
MD
LG