Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Oktoba 01, 2023 Local time: 16:13

Mkasa kanisani wauwa takriban 100 Nigeria


Watu wakitazama paa lililoporomoka la kanisa mjini Uyo, Nigeria

Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kutafuta manusura kwenye vifusi vya kanisa moja kusini mwa Nigeria baada ya paa yake kuporomoka .

Wafanyakazi wa uokozi wanaendelea kutafuta manusura kwenye vifusi vya kanisa moja kusini mwa Nigeria baada ya paa yake kuporomoka na kuuwa takriban watu 100. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa idadi hiyo huenda ikawa 160. Mamia ya waumini walikuwa kwenye kanisa la Reigners Bible Church ambalo bado ujenzi unaendelea wakati paa lake lilipoanguka Jumamosi kwenye mji Wa Uyo.

Kulingana na msemaji wa polisi kutoka eneo hilo Cordelia Nwawe, ni watu 27 waliouwawa huku wengine 30 wakijeruhiwa. Kulikuwa na maafisa kadhaa wa kieneo wakati wa mkasa huo akiwemo Udom Emmanuel ambae ni Gavana wa jimbo la Akwa Ibom alienusurika bila kujeruhiwa.

Mmoja wa waathirika wa ajali hiyo alielazwa hospitali ameviambia vyombo vya habari vya eneo hilo kuwa paa lilianguka nusu saa baada ya hafla kuanza ambapo Gavana aliondolewa haraka ingawa baadhi ya watu hawakubahatika. Gavana Emannuel kupitia ujumbe wa tweeter ametangaza Jumapili na Jumatatu kuwa siku za maombolezo

XS
SM
MD
LG