Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:04

Nigeria: Boko Haram yashukiwa kufanya shambulizi Yobe.


wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika doria nchini humo
wanajeshi wa Nigeria wakiwa katika doria nchini humo

Takriban zaidi ya watu 40 wameuwawa katika shambulizi la kujitoa muhanga kwenye shule kaskazinimagharibi mwa Nigeria, wengi wao wakiwa wanafunzi.

Mlipuko huo ulitokea Jumatatu kwenye mji wa Potiskum katika jimbo la Yobe kaskazinimashariki mwa nchi wakati wanafunzi hao walikuwa wamekusanyika pamoja kwenye shule hiyo ya sekondari inayoendeshwa na Serikali ikifundisha sayansi.

Wafanyakazi wa afya wanasema takriban watu 79 walijeruhiwa kwenye mlipuko wengi wakiwa na hali mbaya.

Mashahidi wanasema mjitoa muhanga alikuwa amevalia sare za shule.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi lakini kuna tetesi kwamba wanamgambo wa kundi la Boko Haramu wanaweza kuwa wamehusika.

Kundi hilo lilishutumiwa kwa kufanya shambulizi kwenye mji wa Potiskum wiki moja iliyopita wakati mjitoa muhanga alipovamia mkusanyiko wa kidini na kuuwa zaidi ya dazani mbili ya watu.

XS
SM
MD
LG