Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Februari 07, 2023 Local time: 21:32

Nigeria yajiandalia 'fainali' ya Kundi D na Argentina


Wachezaji wa Nigeria wakishangilia goli dhidi ya Iceland

Nigeria imejipa nafasi ya kupigania nafasi ya pili ya Kundi D kuingia katika raundi ya pili ya fainali za kombe la dunia kwa ushindi mzuri wa 2-0 dhidi ya Iceland Ijumaa,

Kwa ushindi huo Nigeria imeandaa fainali baina yake na Argentina kuwania nafasi ya pili - nyingine ikiwa tayari imechukuliwa na Croatia - kuingia raundi ya pili kutoka kundi hilo.

Nigeria ina pointi tatu sasa wakati Argentina ina pointi moja. Zitakapokutana katika mechi yao ya mwisho Juni 26 wataamua nani kati yao anaungana na Serbia kwenda raundi ya pili. Argentina inahitaji ushindi dhidi ya Nigeria kumaliza na jumla ya pointi nne, wakati Nigeria ikishinda itamaliza na pointi sita. Endapo timu hizo zitatoka sare Argentina itakuwa nje ya mashindano lakini Nigeria ikiwa na pointi nne italazimika kuangalia matokeo ya Croatia na Iceland kwani Iceland ikishinda itafungana kwa pointi na Nigeria.

Kwa vyoyote vile, zote Nigeria na Argentina zinaangalia mechi yao ya Jumanne kama msitari wa mwisho wa uhai wao - kufa ama kupona.

Argentina imejikuta katika wakati mgumu kwenye mashindano hayo baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na Iceland katika mechi ambapo mchezaji nyota Lionel Messi alikosa penalti. Baada ya kufungwa 3-0 na Croatia matumaini yake yalielekea kudidimia lakini yalifufuka pale Nigeria ilipoifunga Iceland 2-0 Ijumaa. Kwa hiyo hatima ya Argentina ipo mikononi mwake.

Hatima ya Nigeria pia ipo mikononi mwake, ikifahamu wazi kuwa inahitaji ushindi ili kuondoa uwezekano wa timu nyingine yoyote, mbali na Croatia, kupata zaidi ya pointi sita.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG