Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:41

Niger yavipokea vikosi maalum vya Ufaransa na Ulaya


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akutana na wanajeshi wa Barkhane, kikosi kinachoendesha operesheni kubwa zaidi ya Ufaransa nje ya nchi, huko Gao, Kaskazini mwa Mali, Mei 19, 2017.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron akutana na wanajeshi wa Barkhane, kikosi kinachoendesha operesheni kubwa zaidi ya Ufaransa nje ya nchi, huko Gao, Kaskazini mwa Mali, Mei 19, 2017.

Niger imekubali kwamba vikosi maalumu vya Ufaransa na Ulaya vitavuka mpaka wake kutoka nchi jirani ya Mali ili kupambana na makundi ya wanajihadi na kujaribu kuulinda mpaka na taifa hilo la Afrika Magharibi, rais wa Niger amesema katika ukurasa wake wa Twitter.

Katika maelezo yake ya kwanza tangu Ufaransa kusema Alhamisi kuwa itaondoka Mali pamoja na washirika wake wa kijeshi, Rais Mohamed Bazoum alisema vikosi vitaweza kujibu vitisho vya makundi ya wanajihadi katika eneo hilo.

Takriban wanajeshi 2,400 ambao walikuwa sehemu ya wanajeshi waliopelekwa Mali kupambana na makundi yanayo jihusisha na al-Qaida na Islamic State na karibu vikosi maalum 900 katika kikosi cha Ufaransa wanatarajiwa kuondoka Mali katika miezi ijayo.

Niger, Mali na Burkina Faso zimepambana kudhibiti makundi yenye silaha ambayo yameuua mamia ya watu, kuwakosesha makazi mamilioni ya watu na kusababisha maeneo katika eneo la mpaka la Sahel Magharibi mwa Afrika kuwa lisiloweza kutawaliwa.

XS
SM
MD
LG